Watoto nao waliwakilisha Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu. Kulia ni Msafiri Manongi kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
Tuzo hiyo imekabidhiwa na mgeni rasmi Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame na kupokelewa na Mkuu wa Masharika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez.
Umoja wa Mataifa umekuwa kinara wa kuelimisha wananchi, kupitia njia mbalimbali ikiwemo redio, magazeti mitandao ya kijamii na pia kushiriki katika maonyesho ya sabasaba kila mwaka kwa Zaidi ya miaka 6 na kwa miaka 5 mfululizo wamekuwa wakishinda tuzo hizo.
Umoja wa Mataifa mwaka huu umekuja na kampeni ya uhamasishaji wa Malengo ya dunia (Global Goals) na umuhimu wa watanzania kuyaelewa malengo hayo na kuwa mabalozi katika kuhakikisha malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs) yanatekelezeka.
Banda la Umoja wa Mataifa linapatikana katika ukumbi wa Karume yanakoendelea maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa almaarufu ‘sabasaba’ katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni