Timu ya Ureno imekuwa timu ya kwanza
kutinga nusu fainali za michuano ya Euro 2016, baada ya kuitoa Poland
kwa mikwaju ya penati 5-3, kufuatia kumaliza kwa sare ya 1-1 ndani ya
dakika 120.
Shukrani zimuendee Ricardo Quaresma
aliyefunga penati ya ushindi kwa Ureno baada ya penati iliyopigwa na
Jakub Blaszczykowski kuokolewa na Rui Patricio.
Katika mchezo huo Poland ilikuwa ya
kwanza kutikisa nyavu za Ureno kupitia kwa Robert Lewandowski kabla
ya Renato Sanches kusawazisha. Ureno sasa itavaana kati ya Wales na
Ubelgiji.
Ricardo Quaresma akifunga penati iliyoipa ushindi Ureno
Beki wa Southampton Jose Fonte akishangilia huku akiwa amebebwa na Ronaldo mgongoni
PENATI ZENYEWE ZILIKUWA HIVI:-
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni