Wapiganaji wanaodaiwa kuwa wa kundi
la al-Shabaab leo asubuhi wamevamia kituo cha polisi kilichopo
Wajir kaskasini mashariki mwa Kenya na kuiba bunduki na risasi.
Shambulio hilo la kituo cha polisi
cha Diff kilichopo Wajiri Kusini limefanyika majira ya saa saba usiku
na kuwazidi nguvu polisi waliokuwa kwenye kituo hicho.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Joseph
Boinnet amesema wapiganaji hao wa al-Shabaab wapatao 100 wakiwa na
gari lenye silaha nzito pia wamepora kwenye maduka na kumjeruhi
polisi mmoja.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni