Karibu
robo milioni ya watoto katika sehemu ya jimbo la Borno nchini Nigeria
lililokuwa likikaliwa na kundi la Boko Haram wanakabiliwa na
utapiamlo.
Shirika
la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) limesema makumi ya
maelfu ya watoto hao watakufa iwapo hawatofikiwa na huduma za tiba
mapema.
Katika
eneo ambalo wapiganaji wa Boko Haram walikuwa wakilishikilia, UNICEF,
wamekuta watu wakiwa hawana maji, chakula na mazingira machafu.
Mwezi
uliopita shirika la UNICEF lilisema watu waliokuwa wanakimbia maeneo
waliopo Boko Haram wanakufa kwa njaa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni