Kwa upande wa mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Eda Sanga aliwapongeza wanafunzi ambao wamehitimu masomo na wazazi kwa moyo wao wa kujitoa kuwasomesha watoto wao lakini pia kuwataka kuwasimamia vyema watoto wao ili waweze kufika mbali kielimu.
"Elimu ni muhimu sana kwa watoto wenu wanatakiwa kusoma ili kufika mbali kimaisha niwasihi kuwasimia vyema watoto ili wanapokuwa shuleni wafanye vizuri na wanaporudi nyumbani pia wafanye vizuri," alisema Eda.
Kutoka kushoto ni Victoria Martin, Thuwein Makamba na Husni Seif, LTE Specialist wa Tigo Tanzania katika mahafali shule ya Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone.
Wahitimu wakiendelea kutunikiwa vyeti.
Mhitimu Patrick Kasanga akipokea cheti chake.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone, Usia Nkhoma Ledama wakati wa mahali ya nne ya shule hiyo ambapo watoto wa ngazi mbalimbali za madarasa walihitimu.
Usia alisema kuwa wazazi wengi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kujishughulisha na kazi zao bila kuwa na muda wa kukutana na watoto wao na hivyo kuwa ngumu kutambua chanzo cha tabia ambazo zinaibuka kwa watoto wao kutokana na wao kutowafatilia watu ambao wanakuwa karibu na watoto.
"Tunafahamu wazazi wengi mnakuwa busy na kazi zao na hivyo mtoto akitoka shule anakuwa na dada au kuangalia tv lakini akiwa katika michezo na watoto wenzake mnakuwa hamjui ni vitu vya aina gani wanafanya,
"Nadhani ni vyema sasa kuhakikisha mnawafahamu marafiki wa watoto wenu, marafiki zao wa shuleni na marafiki zao wa nyumbani, huwezi kujua wanafanya nini kama huwafahamu tabia watoto wanaocheza nao lakini kama ukiwajua unakuwa unafahamu rafiki anayefaa ni yupi," alisema Usia.
Aidha aliwatoa hofu wazazi kuwa shuleni hapo wanawafundisha watoto tabia njema na wanawafahamu vyema wanafunzi wao hivyo kazi kubakia kwa wazazi kuhakikisha wanakuwa makini na watoto wanapokuwa nyumbani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni