.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 16 Agosti 2016

DIEGO COSTA AIPA CHELSEA USHINDI KATIKA DAKIKA ZA MWISHO


Goli la dakika za mwisho la Diego Costa limempatia kocha Antonio Conte ushindi usiotarajiwa akiwa Meneja wa Chelsea wakati wa mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya West Ham.

Mshambuliaji huyo wa raia wa Hispania alifunga kwa shuti la umbali wa yadi 20 katika dakika ya 89, na kuwafanya mashabiki wa Chelsea wapagawe katika dimba la Stamford Bridge, huku Conte akiungana nao.

Katika mchezo huo ulioishia kwa ushindi wa magoli 2-1, Eden Hazard alikuwa wa kwanza kuifungia Chelsea kwa mkwaju wa mpira wa adhabu baada ya Michail Antonio kumfanyia madhambi Cesar Azpilicueta. Hata hivyo James Collins aliisawazishia West Ham.
   Diego Costa alikuwa na bahati kutopewa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi kipa Adrian
Adrian akiugulia maumivu huku akimuonyesha Diego Costa namna alivyomuumiza na kumsababishia jeraha
       Eden Hazard akiachia shuti lililojaa wavuni na kuiandikia Chelsea goli la kwanza

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni