Meneja wa Huawei nchini Tanzania Bw. Huxiangyang Jacko(Kushoto) akimpatia mshindi David Michael simu ya Huawei P9 Lite katika tamasha la Serebuka Festival’
Meneja masoko wa Huawei nchini Tanzania Bi. Jane Wang(Kushoto) akiteta jambo na mshehereshaji wa tamasha Bi. Jokate Mwegelo katika tamasha la Serebuka Festival’ Asante Sana!!
Dar es Salaam, Agosti 2016; Kufuatia mafanikio makubwa ya tamasha la Bongo Star Search 2015 lililodhaminiwa na kampuni ya Huawei Tanzania, kampuni hii kwa mara nyingine tena imejihusisha na tamasha jingine la muziki lijulikanalo kama Serebuka Festival kama nafasi ya kuonyesha matoleo yake mapya ya simu za Huawei Y6 Pro na P9 lite.
Huawei Tanzania inaona fahari kutangaza ushiriki wake katika tamasha la Serebuka Festival kama mdhamini mkuu wa tamasha hilo. Udhamini huu unaziunganisha bidhaa zake adhimu Huawei Y6 Pro na P9 lite na tamasha hili mashuhuri.
Bi. Jane Wang, Meneja Masoko wa Huawei Tanzania anasema, “Huawei inafaamika kama kampuni ya simu inayoongoza Tanzania, mtazamo unaodhihirisha ubora wetu katika soko la ndani, hata hivyo, tunapenda kujidhihirisha katika maeneo mengine ya kimaisha ili kuwafikia wateja mbalimbali. Tumekuwa kukikutana na mashabiki wapya wa Huawei kupitia mchango wetu katika matamasha ya muziki na vipaji, na umahiri wetu wa kuwasiliana na vijana utaimarika kupitia udhamini huu. Tunaona fahari kushiriki pamoja na Startimes, moja ya visembuzi mashuhuri hapa Tanzania”.
Serebuka Festival ni Tamasha lililoandaliwa na Startimes katika kuadhimisha miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya Startimes linakayofanyika Jumamosi, Agost 13, saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni katika viwanja vya Posta, Kijitonyama. Tamasha hili litajumuisha wasanii maarufu nchini kama vile Yamoto Band, Snura, Jokate, Stamina, Juma Nature, Ali Kiba, Lady Jaydee, Shaa na Madee. Na wengine ni Wema Sepetu, ray, JB na Steve Nyerere. Huawei inaiona hii kama fursa ya kipekee kwa wapenzi wa Huawei kuweza kujumuika na wasanii wa Tanzania.

Kwa kutambua matarajio makubwa waliyonayo wapenzi wa Huawei kuhusiana na kile ambacho Huawei itakileta katika tamasha hili, Huawei inawaahidi wapenzi wa muziki tamasha lililosheni na kutosheleza kiu ya wote watakaohudhuria. Wakifungua toleo lao jipya la simu ya Huawei P9 Lite katika soko la Tanzania, wadhamini hawa watatambulisha bidhaa zao kuu mbili za matoleo ya P9 lite na Y6 Pro, pia kutakuwa na bahati nasibu itakayoendeshwa na kampuni ya Huawei, picha pamoja na wasanii na huduma nyingine nying za kipekee kwa wanatamasha watakao hudhuria.
Huawei Tanzania itakuwa na sehemu ya maonyesho ya simu ambapo wageni wanaweza kugusa na kujipatia hisia ya mguso wa matoleo mapya ya Y6 Pro na P9 Lite.
Akizungumza wakati wa maandalizi ya tamasha hilo Meneja wa Huawei nchini Tanzania Bw. Huxiangyang Jacko alisema “Tukiwa tumetambua uhitaji unaoongezeka wa simu za kisasa katika kundi la watu wa kati nchini wakiwamo vijana, tunaona kuwa tamasha hili limekidhi viwango mahususi vinavyohusiana na bidhaa zetu na soko tunalolihitaji. Tunayo furaha kubwa kutangaza ushirikiano wetu na Startimes katika Serebuka Festival, tamasha litakalowajumuisha wengi wa vijana wa kisasa; ambao ndio walengwa halisi wa Y6 Pro na P9 Lite. Tunafurahi kupata fursa hii ya kudhamini tamasha la namna hii linaliwajumuisha vijana wengi.”
Y6 Pro ni mahususi kwa wale ambao wanahitaji simu inayoweza kukaa muda mrefu bila kuongezewa chaji. Ni miongoni mwa simu pekee zilizo katika kiwango cha thamani yake zinazoweza kuvumilia matumizi makubwa. Y6 Pro inajivunia kuwa na betri yenye nguvu kubwa na huingia chaji kwa haraka sana, kwa dakika 10 tu inaweza kuchaji kutoka 0% hadi kufikia ujazo unaoweza kutumika kwa masaa 3 ya kupiga.
Huawei Y6 Pro si tu ni mapinduzi ya kiteknolojia ya simu za kisasa, bali inamwonekano murua pia. Ikiwa na ukubwa 8.5mm tu, ni simu ambayo huweza kutumika kwa mkono mmoja, kitu muhimu sana kwa watu ambao maisha yao yana pilika pilika nyingi. Y6 Pro inajivunia kuwa na utendaji ambao haupatikani katika simu zingine za kiwango kama chake. Ina uwezo wa kipekee wa kupiga picha ili kunasa matukia muhimu katika pilika pilika.
P9 Lite ni bidhaa bora sana mahususi kwa watumiaji wa kisasa wenye umri katika ya miaka 15 – 35 ambao hupenda kupiga picha na kusikiliza muziki ikiwa na kamera bora sana. Simu hii ina kioo kinachoonesha vizuri chenye teknolojia ya FHD. Inaweza kutumia kadi ya micro CD yenye GB 128 kwa ajili ya nafasi ya kuhifadhi vitu na inauwezo ulioongezewa wa kutambua alama za vidole.
Tamasha hili ni fursa nzuri ya kuweza kuzionesha hizi bidhaa mbili za Huawei P9 Lite na Y6 Pro.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni