Hilo limebainika katika utafiti ulioendeshwa kwenye hifadhi ya misitu na miti huko Suffolk, nchini Uingereza, ambao umebaini pia joto huwafanya senene washindwe kuruka na kuzubaa tu katika majani.
Kabla ya kufanyika kwa utafiti huo, wanandoa wawili wa eneo hilo waliokuwa wamepumzika ufukweni kwa ajili ya kuota jua, walimuona senene mmoja akiwa amezubaa majanini huku mwili wake ukibadirika rangi na kuwa wa pinki
Wanandoa hao walimchukua senene huyo na kumpeleka katika taasisi moja ya utafiti wa wadudu na ndipo utafiti wa awali ulionyesha kuwa senene nao husumbuliwa na joto na miili yao hubadilika rangi na kuchoka wanapopigwa na jua kali au kupata joto kali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni