.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 6 Agosti 2016

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI ATEMBELEA SHIRIKA LA TAIFA LA UTANGAZAJI (TBC)

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba akimkabizi kitabu ta wageni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipotembelea ofisi za Shirika hilo mikocheni mapema leo asubuhi. PICHA ZOTE NA FC GODFREY PETER)
Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (wa kwanza kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi mkuu wa TBC Dk. Ayoub Rioba na wa pili ni Kaimu Kamishna wa Usalama dhidi ya moto Fikiri Salla .
Mkurugenzi wa Matukio wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Bi Martha Swai (wa kwanza kulia) akitoa maelezo jinsi ya upokeaji wa habari za matukio mbalimbali kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (katikati) alipotembelea ofisi hizo mapema leo asubuhi (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Dk. Ayoub Rioba .
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyesimama mbele, akimsomea taarifa ya Jeshi hilo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba alipotembelea ofisi za Shirika hilo mapema leo asubuhi
                                                                                                        Kikao kikiendelea
Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (katikati) akipokea maelezo jinsi ya chumba cha matangazo kinavyofanya kazi (Studio) kutoka kwa Mtangazaji Bi Anna Mwasioke hayupo pichani, (kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa TBC Taifa Dk. Ayoub Rioba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba akimtembeza sehemu mbalimbali mgeni wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipotembelea ofisi za Shirika hilo mikocheni mapema leo asubuhi.
Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (watatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mtangazaji Asha Haji (katikati) alipotembelea chumba cha habari cha Shirika hilo, wa kwanza kushoto ni msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi, akifuatiwa na Mkurugenzi mkuu wa TBC Dk. Ayoub Rioba.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba (aliyesimama mbele) akiwatambulisha wakuu wa vitengo na wafanyakazi wa Shirika hilo, kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyekaa katikati mbele alipotembelea shirika hilo mapema leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba akimtembeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipotembelea ofisi za Shirika hilo mikocheni mapema leo asubuhi.
Kaimu Kamishna wa Usalama dhidi ya moto Fikiri Salla (wa kwanza kushoto walio kaa) akitoa maelezo jinsi ya kutumia kizimia moto cha awali (Fire Extinguisher) uliopo kwenye gari la kurushia matangazo (OB Van)

Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (katikati) akipokea maelezo jinsi ya chumba cha matangazo kinavyofanya kazi (Studio) kutoka kwa Mtangazaji Bi Anna Mwasioke hayupo pichani, akiwa na Mkurugenzi mkuu wa TBC Taifa Dk. Ayoub Rioba

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye afanya ziara Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kwa kumtembelea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dk. Ayub Rioba ili kujifunza na kukuza mahusiano kati ya Taasisi hiyo na Jeshi hilo.

Katika ziara hiyo Kamisha Jenerali, alitembelea ofisi za Shirika hilo zilizopo Mikocheni jijini Dar es salaam, mapema leo asubuhi na alipata fursa ya kujifunza jinsi gani shirika hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kuwa na mazungumzo ya kina na mkurugenzi huyo. “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana na shirika hili ili tuweze kuelimisha umma” alisema Kamishna Jenerali.

Akiwasilisha taarifa ya uendeshaji wa Jeshi hilo Kamishna Jenerali alimueleza changamoto zinazolikabili Jeshi hilo na nia ya yeye kutembelea ofisi hiyo ni kudumisha mahusiano ambayo yatakuwa chachu kwa taasisi hizo kwa manufaa ya umma.

Mkurugenzi wa shirika hilo naye alisisitiza kuwa nivema sasa Jeshi hilo likashirikiana na Shirika hilo ili kutekeleza dhima ya kuokoa maisha na mali, kwa kutumia chombo hicho pamoja na kuwa bajeti ya serikali ni finyu. “Kituo chetu ni cha umma na kwakuwa kazi zetu ni kuisaidia umma wa watanzania tupo tayari kushirikiana”, alisema Mkurugenzi mkuu wa TBC.







Hakuna maoni :

Chapisha Maoni