.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 30 Agosti 2016

KAMPUNI YA TTCL YATJITOSA KUDHAMINI MISS HIGHER LEARNING INSTITUTIONS 2016

Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga akizungumza na washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 pamoja na wageni wengine walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo. Nyuma yake ni washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016
Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga akizungumza na washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 pamoja na wageni wengine walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo. TTCL ndiye mdhamini mkuu wa shindano la Miss Higher Learning Institutions kwa mwaka 2016.

KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) wameingia kama mdhamini mkuu wa mashindano ya urembo kutafuta mrembo toka vyuo vikuu nchini 'TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016' atakaye shiriki katika fainali za urembo kumpata mlibwende wa Tanzania 2016. TTCL wametangaza kuingia katika udhamini huo leo jijini Dar es Salaam ambapo warembo wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 walipotembelea Makao Makuu ya TTCL kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na shirika hilo la umma nchini Tanzania.
 
Akizungumza katika tukio hilo Meneja Huduma kwa Wateja wa TTCL, Aron Msonga alisema shirika hilo limevutwa kusaidia mashindano hayo ili kuweza kuwapata warembo wenye sifa stahiki watakao shinda katika kinyang'anyiro cha 'TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016' na baadaye kushiriki shindano la Miss Tanzania 2016.
 
Alisema TTCL kwa sasa inafanya mageuzi makubwa ya kibiashara na uendeshaji ambayo yameboresha huduma za shirika hilo na bidhaa zake kwa ujumla yanayoinufaisha jamii, hivyo haiwezi kujitenga na shughuli za kijamii ikiwemo mashindano ya urembo. Aidha aliwashauri waandaaji wa TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 kufuata taratibu zote bila upendeleo ili kuweza kuwapata wawakilishi wasomi na wenye sifa za ulimbwende ambao watashiriki vema katika kumpata Miss Tanzania 2016.

 

Kwa upande wake Mratibu wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Bi. Maya Nkiru aliishukuru kampuni ya TTCL kwa kuunga mkono mashindano hayo na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha yanafanyika kwa mafanikio makubwa na hatimaye kupatikana warembo wenye vigezo na sifa kuwakilisha tawi hilo kwa ufasaha.
 
Mratibu huyo alisema shindano la kumpata mrembo atakayewakilisha 'TTCL Miss High Learning 2016' kwa mwaka huu limeboreshwa na litakuwa na burudani za kutosha na utofauti mkubwa hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuweza kushuhudia shindano hilo. Aidha alitaja baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika shindano hilo kuwa ni pamoja na msanii Ney wa Mitego, MB Dog, Msaga Sumu na kundi la QS.
 
TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 itafanyika Septemba 17, 2016 katika Ukumbi wa TTC Chang'ombe jijini Dar es Salaam.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni