.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 1 Agosti 2016

KUNDI LA DOLA YA KIISLAM LAMKATA MKONO CHIFU KWA KUTUMIA KISU

Kundi linalojiita Dola ya Kiislam (IS), limemkamata chifu mmoja na kumkata mkono kwa kutumia kisu kipana huku kundi kubwa la watu likishuhudia unyama huo.

Chifu huyo mwanaume alifunikwa uso wake, aliletwa katika eneo la kati la wazi katika mji unaoshikiliwa na IS wa Raqqa nchini Syria na kulazimishwa kukaa huku mkono wake ukiwa juu ya meza ya mbao.

Picha zenye kuonyesha tendo hilo la kikatili, linawaonyesha wafuasi wa IS waliojifunika nyuso wakiuweka mkono wa chifu huyo kwenye meza hiyo wakijiandaa kuukata kwa kisu kikubwa kwa kutumia chuma.
Wafuasi wa kundi la IS wakiufunga kwa bandeji mkono wa chifu uliokwisha katwa ili kuzuia damu zaidi isimwagike

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni