Timu ya Liverpool imeifunga Arsenal
katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza katika dimba la
Emirates.
Katika mchezo huo Theo Walcott alikuwa
wa kwanza kufunga goli na kuifanya Arsenal iongoze katika dakika ya
31, baada ya kukosa penati.
Philippe Coutinho aliisawazishia
Liverpool kwa mpira wa adhabu alioupiga kwa umahiri, kabla ya Adam
Lallana kufunga la pili baada ya mapumziko.
Coutinho alifunga goli lake la pili na
Sadio Mane kufunga la nne, kabla ya Arsenal's Alex Oxlade-Chamberlain
kufunga goli la jitihada binafsi na Calum Chambers kufunga la tatu
kwa Arsenal.
Adam Lallana akiifungia Liverpool
Sadio Mane akiifungia Liverpool goli la nne
Simon Mignolet akipangua penati iliyopigwa na Theo Walcott




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni