Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akifuatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Annastazia Wambura, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na waombolezaji wengine wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, marehemu Joseph Senga, Sinza Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwenda kwao wilayani Kwimba, Mwanza kwa mazishi kesho.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Waombolezaji wakiiingiza jeneza lenye mwili wa marehemu Senga kwenye gari tayari kusafirishwa kwenda wilayani Kwimba kwa mazishi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Joseph Senga
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akitoa heshima za mwisho
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Joseph Senga
Mjane wa marehemu Senga, Winfrida Senga akiuaga mwili wa mumewe
Mtoto wa marehemu Joseph Senga, Esther akiuaga mwili wa marehemu babake
Mwakilishi wa Chama cha Wapiga Picha za Habari Tanzania, Seleman Mpochi akitoa salamu za rambirambi pamoja na kuwasilisha mchango uliochangwa na wapigapicha kusaidia shuguli za mazishi za aliyekuwa mpiga picha mwenzanoa, marehemu Joseph Senga.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akijadiliana jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
Lowassa akiwa na Nape Nauye pamoja na Freeman Mbowe
Familia ya marehemu Senga
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Tanzania Bara, John Mnyika akitoa salamu za chama hicho
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akitoa salamu za rambirambi
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hizo
Freeman Mbowe ambaye ni mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima, akielezea pengo lililoachwa na marehemu Senga katika gaezeti hilo pamoja na Chadema
Nape Nnauye akitoa salamu za rambirambi za serikali wakati wa kuuga mwili wa marehemu Senga
Nape akaipeana mkono na Lowassa baada ya kutoa salam za rambi rambi
Nape akiteta jambo na Mbowe
Mbunge wa Jimbo la Sumve, wilayani Kwimba, Richard Ndassa, ambaye amewahi fanya kazi na marehemu Senga gazeti la Mfanyakazi, akiuaga mwili wa marehemu Senga
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na baadaye kuhamia Chadema, Mgeja akiauaga mwili wa marehemu Senga
Mhariri Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Julian Msacky akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Senga
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa akitoa heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Senga
Mpiga Picha wa Gazeti la Mtanzania ambaye pia amewahi kufanya kazi na marehemu Senga katika gazeti la Mfanyakazi, Deus Mhagale akiuaga mwili wa marehemu Senga
Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda, ambaye pia amewahi fanya kai na marehemu Joseph Senga gazeti la Mfanyakazi akiuaga mwili wa marehemu
Waombolezaji wakiwemo wanahabari wakiuaga mwili wa marehemu Senga
Wafanyakazi wa Gazerti la Tanzania Daima waliokuwa wanafanyakazi na marehemu Senga wakiwambele ya jeneza la mwili wa Senga
Wapiga picha wakiuingiza kwenye gari mwili wa aliyekuwa mpiga picha mwenzao, marehemu Senga
Baadhi ya wadau waliokuwa miongoni mwa waombolezaji. Kutoka kushoto ni, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, Muhidin Sufiani,Rukia Mtingwa na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanania, Jackson Mmbando
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni