Timu ya Manchester United itakutana
na mshambuliaji wake wa zamani Robin van Persie katika Kundi A la
michuano ya Ligi ya Uropa.
Kikosi hicho cha Jose Mourinho
kitakutana na mshambuliaji huyo Mdachi akiwa na Fenerbahce, pia
kundi hilo zipo timu za Feyenoord na Zorya Luhansk ya Ukraine.
Kwa upande mwingine Southampton,
imewekwa Kundi H, ikivaana na timu yenye fedha nyingi Inter Milan,
Sparta Prague pamoja na Hapoel Be'er Sheva.
Manchester United na Inter Milan zinapewa nafasi kubwa ya kuwa ndio timu zitakazoshinda Ligi ya Uropa kwa mwaka huu
Kwa upande mwingine Mtanzania Mbwana
Samatta akiwa na Genk atakuwa na kibarua kigumu pale watakapovaana
Athletic Bilbao, Rapid Vienna pamoja na Sassuolo katika Kundi F.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni