Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (wa pili kulia, akikagua banda la
Benki Kuu, kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa
Nyamuhongolo Jijini Mwanza, kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, akisaini kitabu cha wageni kwenye
banda la Benki kuu, kwenye maoneshp ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akiteta jambo na Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia)
Mcheza
ngoma wa kikundi cha kutoka Bujora akitumbuiza huku akicheza na nyoka
Na, Binagi Online TV
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa
Biashara Tan-trade kukamilisha ramani ya viwanja vya Nyamuhongolo
vinavyotumika kwa maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane ili
kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu kwenye viwanja hivyo.
Akifungua
rasmi jana maonesho ya Nanenane yanayohusisha mikoa ya Kanda
ya
ziwa, Mongela, alisema kukamilika kwa ramani hiyo kutaharakisha
kuanza kwa ujenzi wa mabanda ya kudumu kwenye viwanja hivyo ili
kuwezesha kuendelea kwa shughuli mbalimbali hata maonesho
yatakapomalizika.
Alisema
mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na mikoa mingine ya kanda ya ziwa,
umejipanga kuandaa maonesho ya Nanenane kitaifa ndani ya miaka miwili
ijayo, hivyo ujenzi wa mabanda hayo utachangia kuongeza hamasha ya
mikoa hiyo kuwa mwenyeji.
Aidha
mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ameungana na mwenzake wa mkoa wa
Shinyanga, Zainab Telack, kuwahamasisha wakulima wa mikoa hiyo
kufufua kilimo cha
pamba ambacho amesema kitachangia kufufua viwanda mbalimbali na
kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana na hivyo kukuza pato la
familia na taifa kwa jumla.
Kwa
upande wao baadhi ya washiriki wa maonesho hayo zikiwemo taasisi za
serikali na wajasirimali, wamesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa
wananchi kutembelea maonyesho hayo tofauti na maonesho ya miaka
iliyopita.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo,
Damian Chang’a, amesema maonesho ya mwaka huu yanashirikisha jumla
ya Halmashauri 18 kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyangana na Mara
huku mikoa ya Simiyu na Kagera ikishindwa kushiriki.
Itakumbukwa
kwamba, alieyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo,
ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, nae aliwahi kutoa ahadi kama
aliyoitoa Mongela, katika Maonesho ya Nanenane miaka iliyopita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni