Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alitembelea eneo la Isimila na kujionea uzuri na mandhari yake. Isimila ni eneo la kihistoria lililopo mkoani Iringa nchini Tanzania, katika kijiji cha Ugwachanya kwenye kata ya Mseke kilichopo kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya. Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa huu wa Iringa.
Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi ilionekana kati yao ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina ya tofauti ya viboko.

Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila ambalo lina mikondo miwili ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji.
Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zama nyingine na Shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu.
Kuna nguzo za kipekee zilizotengenezwa na mmomonyoko wa udongo. dalili zinaonyesha kivutio hiki kinaweza kupotea kutokana na mvua kali zikienyesha miaka ijayo.
Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila ambalo lina mikondo miwili ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji.
Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zama nyingine na Shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni