Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh Richard Kasesela ( aliyeshika mic ) akiendelea na kikao cha usuluhishi
Kiongozi wa kabila Mchanganyiko Bwana Mabula akipena mkono na Laigwani wa kabila la kimasai kama ishara ya kumaliza mgogoro. Na walikubaliana watachinja ng'ombe na kuwaita watu washiriki katika hafla ya umoja.
Hali ya sintofahamu kati ya wafugaji jamii ya kimasai na wale wa makabila mengine iliisha baada ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela kusuluhisha mgogoro huo ambapo pande zote mbili zilikubaliana kuunganisha nguvu ya ulinzi shirikishi.
Mwanzoni Mkutano ulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani kwani makundi yote mawili yalikuja na silaha za jadi huku wakiwa na jazba.
Chanzo cha mgogoro huo ni wizi wa mbuzi zinazosadikiwa kuibiwa na kijana wa kimasai aitwaye Maneno Ndimbau akishirkiana na mtuhumiwa ajuliknaye kwa jina moja tu Baraka ambaye tayari amekamatwa.
Jumatatu tarehe 29/08/16 makundi haya yatakutana na kuunganisha nguvu kupambana na uhalifu na wizi wa mifugo.
Akiongea na wafugaji hao, Mkuu wa wilaya alisistiza kuwa " ubaguzi wa kikabila ni jambo hatari sana sio jambo la kuliachia likakua, ni marufuku kwa mtanzania kubagua kabila lingine tanzania ni moja sote tu wamoja"
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni