Zlatan
Ibrahimovic ametikisa nyavu mara mbili na kuipa ushindi wa nyumbani
Manchester United wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Southampton
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Mshambuliaji
huyo hatari raia wa Sweden aliwanyanyua mashabiki wa Manchester
United katika dimba la Old Trafford baada ya kuupiga kichwa mpira wa
krosi iliyopigwa na Wayne Rooney na kuandika goli la kwanza.
Ibrahimovic
alifunga goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Jordy Clasie
kumuangusha beki wa Manchester United Luke Shaw. Paul Pogba
aliyevunja rekodi ya uhamisho wa paundi milioni 89 alicheza kwa mara
ya kwanza na kuonyesha uwezo wake.
Ibrahimovic na Paul Pogba wakiangalia mpira wa kichwa ukielekea wavuni na kuipatia Manchester United goli la kwanza
Zlatan Ibrahimovic akijipinda kuachia shuti la mpira wa penati uliojaa wavuni na kuandika goli la pili



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni