Mwanariadha wa Haiti Jeffrey Julmis
ambaye alianza kwa mikwara ya kuiga ishara ya Usain Bolt katika mbio
za kuruka vihunzi amejikuta akigonga kihunzi cha kwanza na kuanguka
chini.
Mikwara ya mwanariadha huyo
iliwavutia watazamaji na kujikuta wakimfuatilia kwa umakini mbio
zilipoanza hata hivyo mbwembwe zake ziliishia katika kiunzi cha
kwanza tu.
Mwanariadha wa Haiti Jeffrey Julmis akiwa chini baada ya kugonga kihunzi cha kwanza katika michuano ta Olimpiki Rio
Mwanariadha Jeffrey Julmis akijizoa zoa kunyanyuka baada ya kuanguka



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni