Neymar amefunga katika sekunde ya
14, likiwa ni goli la mapema mno kufungwa katika historia ya michuano
ya Olimpiki, wakati Brazil ikiichakaza bila huruma Hondura kwa magoli
6-0 na kutinga fainali.
Wenyeji Brazil watakutana na
Ujerumani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa magoli 7-1 katika kombe la
dunia 2014, hii ni baada ya kuitoa Nigeria kwa magoli 2-0
yaliyofungwa na Lukas Klostermann na Nils Petersen.
Katika ushindi huo uliofufua
matumaini kwa Brazil kutwaa ubingwa, Neymar na Gabriel Jesus
walifunga magoli mara mbili.
Neymar akifunga goli la kwanza ndani ya sekunde 14 tu ya mchezo
Neymar akiwa angani akiuangalia mpira ukiingia golini
Neymar akigugumia maumivu ya kifua baada ya kuangukia kifua wakati wa kufunga goli hilo




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni