Neymar
amefunga penati ya ushindi wakati wenyeji Brazil wakiifunga Ujerumani
kwa magoli 5-4 kwa mkiwaju ya penati Jijini Rio na kushinda medali
yao ya dhahabu ya Olimpiki katika mchezo wa soka wanaume.
Katika
mchezo huo mkali timu hizo zilijikuta zikitoka sare yagoli 1-1 baada
ya muda wa nyongeza, huku goli la mpira wa adhabu lililofungwa na
Neymar likisawazishwa na Max Meyer.
Ushindi
huo wa Brazil umekuja baada ya Ujerumani kuichakaza Brazil magoli 7-1
mwaka 2014 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Duniani katika
dimba la Belo Horizonte nchini Brazil.
Neymar akifunga mpira wa penati ulioipa ushindi Brazil
Neymar akishangilia goli kwa kuonyesha ishara inayotumiwa na mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt
Mwanariadha wa Jamaica Mfalme wa Riadha Usain Bolt akifuatilia mchezo huo.
Nayo
timu ya taifa ya Nigeria imeshinda medali ya fedha katika michuano ya
Olmpiki ya soka la wanaume baada ya kuichakaza bila huruma timu ya
Hondura kwa mgoli 3-0 yaliyofungwa na Sadiq Umar mawili na Aminu Umar
moja.




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni