.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 10 Agosti 2016

SERIKALI YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI MOI

pix 1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza mbele ya watumishi wa Taasisi ya mifupa muhimbili (MOI) hawapo pichani wakati alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi ha oleo jijini Dar es salaam.
pix 2
Kaimu Mkurugenizi wa MOI Dkt. Othman Kiloloma akizungumza mbele ya watumishi wa Taasisi ya mifupa muhimbili (MOI) hawapo pichani kabla ya kumkaribisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi hao leo jijini Dar es salaam.
pix 3
pix 4 pix 5
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya mifupa muhimbili (MOI) wakitoa kero zao mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi hao leo jijini Dar es salaam
pix 6
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya mifupa muhimbili (MOI) wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi hao leo jijini Dar es salaam.

Serikali chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa siku 14 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) Dkt. Othman Kiloloma kukaa na bodi ya taasisi hiyo kushughulikia matatizo ya watumishi ili kuleta ufanisi mzuri katika kitengo hiko.

Akizungumza na watumishi wa MOI Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemtaka Dkt. Kiloloma kukaa na bodi ya taasisi hiyo ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya watumishi wake ndani ya siku 14 ili wafanyakazi waweze kutoa huduma bora kwa watanzania.

“Naagiza Bodi ya MOI pamoja na Kaimu Mkurugenzi wake ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya watumishi wake ndani ya siku 14 ili kuondoa malalamiko na kuleta ufanisi bora katika taasisi hii”alisisitiza Mhe. Ummy.

Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa amepokea changamoto zao na za taasisi hyo nakuhaidi kuzitatua ndani ya mwezi mmoja na kuwataka wasichoke kutoa huduma bora kwa watanzania ili kuokoa maisha yao na kupambana na umaskini.

Mbali na hayo Mhe. Ummy ameagiza watendaji wa Wizara yake kuleta mkakati wa kupambana na kupunguza ajari za barabarani hasa zitokanazo na bodaboda ndani ya siku 14 ili kuwapa nafuu madaktari na wauguzi wa MOI kuweza kuondoa mlundikano wa wagonjwa hospitalini hapo.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi MOI Dkt.Othman Kiloloma amesema kuwa mbali na changamoto wanazokutana nazo wamefanikiwa kuunda upya wafanyakazi wataoweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa jumamosi na itaanza mara moja.

Aidha Dkt. Kiloloma ameongeza kuwa MOI imeweza kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 1.1 kwa mwezi kutoka kiasi cha shilingi milioni 400 kwa kipindi kilichopita.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni