.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 26 Agosti 2016

SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI, MH. ZUBEIR AHUDHURIA MKUTANO WA CPA MAURITIUS

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid yuko nchini Mauritius kuhudhuria Mkutano wa 47 wa Umoja wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afirika (CPA African Region).

Mkutano huo ulioanza Ogasti 22 na kutarajiwa kumalizika Ogasti 27 unafanyika katika hoteli ya Intercontinental Balaclava Mauritius ambapo unahudhuriwa na washiriki wapatao 400 kutoka nchi wanachama 20, chini ya mwenyeji wao Spika wa nchi hiyo Bibi Santi Bhai Hanoomajee ambae kwa sasa ndie Rais wa Jumuiya hiyo kikanda.

Tanzania, Afrika ya Kusini , Msumbiji, Uganda na Kenya ni miongoni mwa nchi zinazoshikiriki katika mkutano huo ambapo pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid, mshiriki mwengine kutoka Zanzibar ni Mwakilishi wa Tunguu Mheshimiwa Simai Mohammed Mpakabasi .

Miongoni mwa mada zinazojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ikiwa ni miongoni mwa mkakati wa kupunguza umasikini pamoja na nafasi ya Mabunge katika kudumisha haki, amani na ushiriki mzuri wa jamii katika shughuli za kisiasa.

Mada nyengine zinazozozungumzwa ni ustawi wa jamii kiafya, kimazingira na kielimu pamoja namaendeleo ya vijana na kuichumi miongoni mwa nchi wanachama.

Awali Mheshimiwa Spika Zubeir na Mheshimiwa Simai Mpakabasi walihudhuria Mkutano wa Kamati Tendaji ambao ulipitia agenda mbali mbali za Mkutano Mkuu.

Zanzibar ni mwanachama wa CPA African Region, ambapo Baraza la Wawakilishi limekua likishiriki mara kadhaa katika mikutano, semina na mafunzo yanayoandaliwa na jumuiya hiyo.

Imetolewa na
Divisheni ya Uhusiano,
Baraza la Wawakilishi,
Zanzibar.
August 25, 2016

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni