Zoezi
la uchangiaji Damu likiendelea katika makao makuu ya TAZARA ambapo
wafanyakazi mbalimbali wa Shirika hilo na watanzania wengine
wamejitokeza kucnagia damu (PICHA NA EXAUD MTEI MSAKA HABARI)
|
Akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa Damu uliopo Tanzania wao kama TAZARA wameamua kusitisha shughuli za leo kwa ajili ya kufanya zoezi moja la kuchagia damu zoezi ambalo linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi
mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU akizngumza na wanahabari
wakati wakiendelea na zoezi la ucnagiaji wa Damu
|
Aidha mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhitaji mkubwa damu kutokana na kuongezeka kwa maswala mbalimbali yakiwemo ya ajali,vifo vya mama na watoto wakati wa kujifungua wanaofariki kwa kukosa damu,na magonjwa mengine mengi hivyo akawataka watanzania kujitahidi na kuhakikisha kuwa angalau wanachangia damu kwa mwaka japo mara mbili ili kuokoa maisha ya watanzania wenzao.
Mmoja
kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa Taifa wa Damu salama Tanzania
Bi Mariam Juma akifafanua jambo juu ya umuhimu wa kucnagia Damu kwa
watanzania
|
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni