Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue mafunzo hayo ya siku tano. Waliokaa ni Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uzalishaji, Tume ya Mipango (katikati) na Bw. John Mduma, Mhadhiri Mwanamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Jijini Mwanza katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi (Veta).
Mgeni Rasmi Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uzalishaji, Tume ya Mipango (aliyesimama) akitoa hotuba kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Rasilimali za Umma kwa washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Geita and Simiyu. Wengine ni Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (kushoto) na Bw. John Mduma, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia).
Washiriki wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Rasilimali za Umma kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Geita and Simiyu pamoja na wawezeshaji wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Muwezeshaji Dr. Kenneth Mdadila, Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akishusha nondo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Picha zote Na: Thomas Nyindo
Tume ya Mipango
Tume ya Mipango
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni