.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 20 Agosti 2016

USAIN BOLT ASTAAFU MICHUANO YA OLIMPIKI KWA KUWEKA REKODI

Mwanariadha Usain Bolt aliyetangaza kutoshiriki tena michuano ya Olimpiki, ameweka rekodi kwa kupata ushindi wa medali tatu za dhahabu na ya tisa katika michuano hiyo wakati Jamaica ikishinda mbio za kupokezana vijiti watu wanne Jijini Rio.

Kabla ya ushindi huo Bolt, 29, alishashinda medali za dhahabu katika mbio za mita 100, na 200, na sasa amekuwa mwanariadha pekee mwanaume kushinda medali tatu za dhahabu mfululizo katika michuano mitatu ya michezo ya Olimpiki.

Bolt alishirikiana na Asafa Powell, Yohan Blake na Nickel Ashmeade ambapo walimaliza kwa kutumia sekunde 37.27. Katika mbio hizo Japan walishangaza ulimwengu kwa kutwaa medali ya fedha na Canada shaba.
      Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt akikatiza katika mstari wa kumaliza mbio hizo
Wanariadha wa Jamaica Usain Bolt, Asafa Powell, Yohan Blake na Nickel Ashmeade wakifurahia ushindi wao 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni