Watoto wachanga wa mwezi mmoja
walioungana mwili waliohamishwa kutoka kitongoji cha wasi
kilichozingirwa na wanajeshi nchini Syria na kupelekwa Jijini
Damascus wamefariki dunia.
Mapacha hao Nawras na Moaz walikuwa
wameungana kifuani na mioyo yao ikiwa katika eneo moja.
Serikali ya Syria iliruhusu
kuondolewa kwa mapacha hao katika eneo la waasi na kupelekwa hospitali Agosti 12, baada ya
madaktari kapaza sauti zao ili kunusuru maisha yao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni