.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 10 Agosti 2016

WAZIRI AWATAKA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALINI KUFANYA KAZI KIMKAKATI

HAS1
Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Zhao Qizheng akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas kitabu cha Shanghai Pudong Miracle kinachoonesha jinsi mji wa Shanghai ulivyotoka kuwa mji wa hali ya chini hadi kufikia mji wa kisasa na wenye maendeleo, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini baina ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini na Waziri huyo leo Jijini Dar es Salaam.
HAS2
Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng akiongea na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kuhusu umuhimu wa Serikali kuwasiliana kimkakati na wananchi na namna bora ya kuwasilisha taarifa kwa jamii, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas.
HAS3
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhao Qizheng, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, Leo Jijini Dar es Salaam.
HAS4
HAS5
Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam.
HAS6
Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam.
HAS7
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas akiongea na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi baina ya Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa China Zhao Qizheng na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini.

                                                                                              Frank Mvungi-Maelezo

Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kufanya kazi zao kimkakati ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao hasa kwenye kipindi hiki cha Awamu ya Tano.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisi za Serikali Waziri wa zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa China, Mhe. Zhao Qizheng amesema ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha kuwa mawasiliano yote yanalenga kuwainua wananchi wake.

“Msemaji wa Serikali inabidi uwe makini katika kazi zako kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati”, alisema Qizheng.

Akifafanua Mhe. Qizheng amesema kuwa ili Tanzania Iweze kufikia maendeleo ya kweli ni muhimu kujenga mfumo dhabiti wa Mawasiliano ya Serikali kwa Umma.

Katika kutekeleza majukumu yao Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kama wasemaji ni lazima wawe na uelewa mpana kuhusu masuala yanayohusu sekta wanazosimamia ili kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi.

Pia aliwataka Wasemaji wa Serikikali kujiandaa kabla ya kujibu hoja mbalimbali za kitaifa na Kimataifa zinazohusu Serikali na wananchi ili kutoa taarifa sahihi kwa Vyombo vya haabari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Hassan Abbas amesema ni dhamira ya Serikali kuwasiliana kimkakati ili kuchochea maendeleo.

“Lengo letu ni Kuhakikisha kuwa tunafanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa mawasiliano ya Serikali na wananchi ili kuwapa fursa ya kutoa mrejesho”alisema Abbas.

Katika kuhakikisha azma hiyo inatumia Abbas amebainisha kuwa kwa sasa Serikali inajipanga kufanya maboresho ya mifumo ya Mawasiliano ya Serikali.

Aidha Mawasiliano ya Serikali katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya Tano yanalenga kubadilisha maisha ya wananchi kutoka hali duni kwenda kwenye hali bora.

Mkutano kati ya Waziri wa Zamani wa Habari wa China na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisis za Serikali umelenga kujenga uwezo wa Wasemaji wa Serikali ili waweze kuwasiliana na Wananchi kimkakati.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni