Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia maendeleo ya nchi hizi mbili.
Pia Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kumpa salamu za pole kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi karibuni.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2016
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni