.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Septemba 2016

BAA LA NJAA: WAPINZANI NCHINI ZIMBABWE WANYIWA CHAKULA CHA MSAADA

Chama tawala nchini Zimbabwe kimetuhumiwa kwa kuwanyima kwa makusudi msaada wa chakula wananchi wanaounga mkono upinzani katika maeneo yenye baa la njaa kutokana na ukame nchini humo.

Tume ya Haki za Binadamu ya Taifa hilo imesema wapinzani wameambiwa na chama cha rais Robert Mugabe cha Zanu-PF kwamba hawatopatiwa chakula cha msaada.

Rais Mugabe alitangaza hali ya tahadhari mwezi Februari, huku serikali ikikadiria watu milioni nne watahitaji msaada wa chakula ifikapo Januari 2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni