Mwanamke mmoja amekufa na raia
wengine 20 wa kigeni wamejeruhiwa baada ya boti walilokuwamo kutokea
mlipuko wa moto hii leo wakati wakitokea Bali Mashariki kwenda kisiwa
cha Gili.
Boti hiyo ya mwendo kasi ya Gili Cat
2, ilikuwa na abiria 40 inaowapeleka kwenye eneo maarufu la watalii
kwa ajili ya mapumziko katika kisiwa cha Gili Trawangan wakati tanki
la mafuta lilipolipuka.
Abiria 20 waliojeruhiwa kwenye boti
hiyo ya mwendo kasi wanatokea mataifa ya Ureno, Ujerumani, Austria
pamoja na Uingereza, ambapo imeelezwa mwanamke aliyekufa ni raia wa
Ujerumani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni