.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 16 Septemba 2016

CITY vs PRISON,MAANDALIZI YAMEKAMILIKA

ZIKIWA zimebaki saa chache kabla ya kuchezwa kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara unaozikutanisha Mbeya City Fc na Tanzania Prison,maandalizi kuelekea mchezo huo uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa yamekamilika.

Akizungumza mbele ya wana habari muda mchache uliopita, afisa habari wa City, Dismas Ten, amesema kuwa maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo huo uliopangwa kuchezwa jumamosi hii saambamba na michezo mingine mitano itakayorindima kwenye viwanja tofauti tayari yamekamilika na kinachosubiliwa na dakika 90 hiyo kesho.

“Kesho ni siku ya mchezo, kwetu sisi huu ni mchezo muhimu kwa sababu tunahitaji kushinda ili tuendelee kuwa kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi, maandalizi ya kutosha yamefanyika kwa hiyo ni nafasi kwa mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kusapoti timu yao,jopo la madaktari wetu limenithibitishia kuwa Geoffrey Mlawa hatakuwepo uwanjani hiyo kesho lakini nyota wengine wako kwenye hali nzuri, huu ni msimu ambao City inarudi kwenye zama zake” alisema.

Kuhusu utulivu na amani uwanjani kwa mashabiki watakaojitokeza kushuhudia mchezo huo, Ten alisema kuwa watu wanatakiwa kuzingatia amani kwa sababu mchezo wa soka hukutanisha watu wengi hivyo ni vyema mashabiki kushangilia timu zao huku wakiwa kwenye hali nzuri ya amani.

“Mashabiki wa City wajitokeze kwa wingi, wasiwe na shaka ya utulivu kwa sababu ulinzi utakuwepo wa kutosha, amani mchezoni ni jambo jema hivyo kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake kuhakikisha tunashangilia timu yetu vizuri katika kuhanikiza ushindi huku tukiwa na wingi wa amani” alimaliza.

City inakutana na Prison huu ukiwa ni mchezo wa 7 kwenye mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara huku rekodi zikionyesha kuwa City imepata ushindi mara 2, Prison wakishinda mara 3 na mara 1 timu hizi zikienda sare, Kiungo Peter Mapunda ndiye mchezaji anashika rekodi ya kufunga bao la kwanza kabisa kwenye mechi zilizokutanisha timu hizi mbili akifunga bao hilo kwenye mchezo wa duru ya kwanza msimu wa 2013/14 kwenye ushindi wa 2-0, misimu itatu iliyopita.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni