Magari yanayotoa huduma za usafiri kwa wanafunzi yakiwa shuleni hapo walimu wakiwa kwenye maafali hayo. Wahitimu wa darasa la saba wakiimba wimbo wa shule. Wanafunzi wa darasa la tatu wakiimba kwenye maafali hayo. Wanafunzi wakiimba wimbo wa kuwaaga darasa la saba. Majadiliano meza kuu na mgeni rasmi. Kulia ni Mchungaji Elisifa Kephasi na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Nipael Mrutu. wanafunzi wa darasa la pili wakitoa burudani. Hapa ni furaha tupu kwa wanafunzi wa darasa la pili baada ya kutoa burudani.
Sarakasi zikifanyika katika maafali hayo. Wageni waalikwa, wazazi na walezi wa watoto hao wakijumuika na watoto wao kwenye maafali hayo.
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila amesema urithi pekee wa watoto ni elimu na sio mali kama ilivyozoeleka.
Kafuli ametoa kauli hiyo katika maafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School Dar es Salaam leo mchana.
"Napenda kuwaomba wazazi na walezi kuendelea kuwapa elimu watoto wenu kwani ndio msingi wa maisha yao badala ya kuwarithisha magari, nyumba na vitu vingine vya thamani" alisema Kafulila,
Kafulila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maafali hayo alitoa shukurani zake kwa uongozi mzima wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwaandaa wanafunzi hao ambao watakuja kuwa wataalamu na viongozi wa baadae.
Mkuu wa Shule hiyo, Felister Mrutu alisema shule yao imekuwa ikipokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali bila ya kujali dini wala uraia na inazingatia maadili jambo linalowavutia watu wengi kuwapeleka watoto wao wakiwemo wa kutoka nje ya nchi.
Katika maafali hayo wanafunzi wa shule hiyo walionesha burudani mbalimbali kama kuimba, gwaride, sarakasi, karate na michezo mingine ya ukakamavu waliyofundishwa na vijana kutoka chama cha Skauti Tanzania.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni