.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Septemba 2016

KAMPUNI YA MAGAZETI YA THE GUARDIAN LIMITED YADHAMINI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian Limited, Richard Mgamba ( katikati ) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kampuni hiyo kudhamini mashindano ya Miss Tanzania 2016. Kulia ni Mkurugenzi wa Lino Agency waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundega na kushoto ni mjumbe wa kamati hiyo Mary Eammanuel
Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga akizungumza wakati Kampuni ya The Guardian Limeted ilipotangaza kudhamnini mashindano ya Miss Tanzania 2016. Kulia kwake ni mjumbe wa kamati hiyo Mary Eammanuel akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian Limited, Richard Mgamba. Wengine ni mkuu wa Itifaki Albert Makoye ( mwenye tai ) na mjumbe Shah.

Kampuni ya magazeti ya The Guardian Limited imejitosa kuyadhamini mashindano ya Miss Tanzania 2016 ambayo yanaandaliwa na kampuni ya Lino International Agency Limited. 

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian Limited, Richard Mgamba amesema kampuni hiyo imeamua kudhamini mashindano hayo kutokana na ubora wake, na pia kupitia mashindano hayo baadhi ya washiriki huonyesha vipaji vyao. 

" Sisi kama chombo cha habari moja ya malengo yetu ni kutoa habari, burudani, kudumisha utamaduni na kusimamia yale yote mazuri yanayoleta amani na mshikamano katika nchi yetu, alisema Mgamba ambaye kampuni yake ni wachapishaji wa magazeti ya The Guardian, The Guardian On Sunday, Nipashe, Nipashe Jumapili, Taifa Letu na Sema Usikike. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency Limited, Hshim Lundega aliishukuru The Guardian kwa kujitokeza kudhamini mashindano hayo na kusema mwaka huu wameyaboresha zaidi na watanzania watarajie shindano lenye msisimko wa kipekee.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni