Timu ya Celtic imepata pointi yake
ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuweza kutoshana
nguvu na Manchester City kwa matokeo ya magoli 3-3 katika mchezo
uliochezwa Glasgow.
Wenyeji waliongoza mara mbili katika
kipindi cha kwanza, kupitia kwa Moussa Dembele aliyebadilisha
muelekeo mpira wa kichwa wa Erik Sviatchenko na Kieran Tierney
kusababisha Raheem Sterling kujifunga.
Shambulizi la Fernandinho liliifanya
Manchester City kusawazisha na kisha Raheem Sterling alionekana
kutulia na kufunga goli la pili, hata hivyo Dembele tena akafunga la
tatu kabla ya Nolito kusawazisha.
Moussa Dembele akifunga goli kwa staili ya aina yake
Nolito akifunga goli la tatu lililoifanya City iepuke kipigo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni