Manchester United imecheza mpira
mbovu katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Uropa na kujikuta
ikipata kipigo cha goli moja kwa bila kutoka kwa Feyenoord.
Jose Mourinho alifanya mabadiliko
manane kutoka katika kikosi kilichofungwa na Manchester City na
nafasi pekee katika kipindi cha kwanza ilipotezwa na Anthony Martial
aliyepiga nje.
Zlatan Ibrahimovic aliingia kutokea
benchi na kupiga nje ya goli mpira wa kichwa. Ilikuwa ni Nicolai
Jorgensen, aliyeotea ndiye aliyeipatia goli Feyenoord akiunganisha
krosi ya Tonny Vilhena.
Nicolai
Jorgensen akifunga goli pekee katika mchezo huo
Paul Pogba aliyenunuliwa kwa paundi milioni 100 bado hajaweza kuonyesha cheche zake
Marcus Rashford akiruka kichwa ambacho hata hivyo mpira ulitoka nje
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni