.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Septemba 2016

MAZOEZI YAMEANZA,MLAWA NJE

BAADA ya mapumziko ya siku ya jana yaliyotolewa na kocha Kinnah Phiri kufuatia safari ndefu ya saa nyingi kutoka kanda ya ziwa, kikosi cha Mbeya City fc leo kimeanza mazoezi rasmi kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa siku ya jumamosi.

Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo afisa habari wa City, Dismas Ten amesema kuwa nyota wote 30 ikiwa ni pamoja na 25 waliokuwa nje ya jiji la Mbeya kwa takribani wiki tatu kwa ajili ya michezo ya mwanzo wa msimu wamejumuika kwenye mazoezi ya leo kwenye uwanja wa Sokoine kwa ajili ya matayarisho ya mchezo huo wa mwishoni mwa juma.

“Tumeanza mazoezi leo, baada ya mapumziko ya siku ya jana,nyota wetu wote wapo ikiwa ni pamoja na wale ambao hawakusafiri na timu kwenda Mwanza na Shinyanga kwenye michezo mitatu ya Mwanzo wa msimu ambayo tuliikamilisha kwa kushinda miwili na suluhu moja,limekuwa ni jambo jema kwetu kwa sababu morari imeongezeka kikosini na kila mmoja yuko tayari kwa mchezo wa mwishomi mwa juma” alisema.

Akiendelea zaidi Ten alisema kuwa huu ni msimu ambao City imejipanga kuvunja rekodi zote ambazo ilikuwa haijawahi kuzifikia tangu ilipopanda daraja misimu mitatu iliyopita.

“Huu ni msimu ambao kwetu utakuwa na kumbukumbu nzuri kwa sababu tumejipanga kufuta ‘madeni’ yote tuliyokuwa nayo, tangu tumepanda daraja tulikuwa hatukuwahi kuongoza ligi hili sasa limeshakwisha,tunasubiri kuvunja rekodi ya kutokuzifunga Yanga na Azam fc jambo ambalo tuna amini tunalianza wikiendi hii” alitamba
Geoffrey Mlawa, mazoezini leo, alipokuwa akijaribu kufanya mazoezi mepesi baadae ripoti ta daktari imesema haweza kucheza mchezo wa jumamosi dhidi ya Azam Fc kwa sababu bado ni majeruhi. 

(Picha nyingine za mazoezi ya leo ziko hapa: https://www.facebook.com/MbeyaCityCouncilFc

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni