.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 27 Septemba 2016

MBONI AWAPIGA MSASA VIONGOZI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA

 Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita akiwafunda wajumbe wa baraza kuu la UVCCM mkoa wa Arusha
  Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wajumbe waliouthuria mkutano huo
Mjumbe wa Kamati ya utelelezaji Taifa kutoka Mkoa wa Lindi
Amir Mkalipa akiwaasa wajumbe waliouthuria katika mkutano huo
  Wa kwanza kushoto ni katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka pamoja na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita wakisikiliza baadhi ya mambo yalikuwa yakiongelewa katika kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa CCM mkoa wa Arusha
                                          Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kikao kwa makini

                                                                               Na Woinde Shizza, Arusha

Viongozi na watendaji wa Jumuiya ya vijana (UVCCM)wametakiwa kutii kanuni na kuongoza kwa uaminifu ili kuheshimu taratibu zilizowekwa chini ya misingi ya nidhamu maadili na kufuata miongozo ya jumuiya na Chama Cha Mapinduzi .

Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita Mara tu alipowasili mkoani Arusha kukutana na kamati ya utekelezaji ya mkoa na kufungua kikao cha Baraza kuu la UVCCM Mkoa wa Arusha vilivyofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa hapa Mboni aliwakumbusha viongozi wa UVCCM nchini kupitia viongozi wa Arusha huku akisiaitiza Chama Cha Mapinduzi ni taasisi inayoheshimika kitaifa, kikanda na kimataifa hivyo kila mwana jumuiya anapaswa kulinda hadhi ya chama hicho mahali popote
 

Alisema CCM si chombo kidogo kama ambavyo baadhi ya watu wanavyokichukulia huku akisema chama hicho ni kikongwe katika siasa Barani Afrika, kikapata heshima na sifa duniani kwa sera , muundo na misimamo yake katika kupigania haki na harakati za ukombozi Afrika na nyingine duniani.
 

"Nasisiitiza hatutakuwa tayari kumkubalia, kumsamehe au kumfumbia macho
mwana jumuiya au kiongozi yeyote ambaye anataka kuipaka matope jumuiya yetu ili itafsirike na kuonekana ni genge la maharamia au waganga njaa kwa
uzembe na tamaa binafsi " alieleza Mboni .

Alisema mwanajumuiya au kiongozi ambaye hatafuata kanuni zilizopo na
atakayeshindwa kuheshimu katiba ya chama, akipindisha miongozo au taratibu tulizowekwa , ajiweke pembeni mapema kwasababu ccm hakitapata hasara aidha kwa kujiengua kwa mwanachama au kwa kuenguliwa.
 

"Jumuiya yetu inayoheshimika, ndiyo tanuru na benki ya viongozi wa kisiasa
na utawala; hatuwezi kwenda kinyume na taratibu tulizojipangia tukaonekana kama kundi la kondoo lisilo mchungaji au halina utaratibu
unaoeleweka" alisisitiza Makamu huyo Mwenyekiti

Alisema amelezimika kuja Mkoani Arusha kuwaeleza viongozi na wanachama
kwamba kila mwanachama au mtendaji anahitaji kubadilika na kujiendesha
kinidhamu kulinda hadhi ya chama na isifikiriwe UVCCM si kijiwe cha
mitafaruku kwa mtu anayetaka kuivuruga jumuiya.

Aidha Mboni alisema kinachohitajika ndani ya UVCCM kwa wakati huu ni
kuendeleza mshikamano, umoja, upendo na nidhamu na anayetaka kuuufanya
uhuni kuwa sehemu ya siasa afanye nje ya jumuiya , bila kuuhamishia utovu
huo wa nidhamu ndani ya jumuiya .
 

"Mwanachama au kiongozi ambaye anataka kuendesha jumuiya kwa msingi ya
uhuni na uchepe alisema ataielewa UVCCM , hapa si mahali pa mazingaombwe ya kihunihuni . tunahitaji matendo ya utii wa kanuni na taratibu ili kupambana na tishio lolote la uasi au usaliti.  


Aliwataka watendaji waliopewa dhamana za utumishi na utendaji waanze
kufanya kazi za jumuiya kwa kutazama mipaka na wajibu wa kikanuni ili
kulinda mali na rasilimali za jumuiya mithili ya mboni za macho yao
"fichueni na watendaji wanaotuhujumu na ikiwa mna ushahidi, watajeni
viongozi wanaotufisidi, wanaotuhujumu na kukwapua mali za jumuiya.
Msiwapakazie watu kwa majungu, chuki au kutaka kuwakomoa na kuwavunjia
heshima zao kwa maneno ya kutungatunga "alisema Mboni

Katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka na mjumbe wa Kamati ya utelelezaji Taifa kutoka Mkoa wa Lindi Amir Mkalipa.
 

Kwa upande wake katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa UvCCM ina miaka 38 sasa ikiwa na heshima ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania hivyo hivyo ili kuifanya UVCCM kuendelea kuheshimika wanachama wanatakiwa kuwa na umoja na mshikamano ndio silaha pekee iliyobakia

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni