Mchezaji Gofu mkongwe nchini
Marekani Arnold Palmer (87) ambaye inaaminika kuwa ni mmoja wa
wachezaji bora zaidi katika historia ya mchezo huo amefariki dunia.
Palmer amefariki dunia kwenye
hospitali ya UPMC Presbyterian huko Pittsburgh, Pennsylvania, ambako
alikuwa akifanyiwa vipimo vya moyo.
Chama cha Gofu Marekani
kimethibitisha kifo cha Palmer kupitia akuanti ya twitta, huku
kikiandika kuwa “alikuwa balozi mkubwa wa mchezo wa gofu”.
Arnold Palmer akicheza michuano ya kombe la Ryder mwaka 1961


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni