Tuzo aliyotunukiwa mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 jijini New York nchini Marekani katika hotel ya St. Regis, New York. African Leadership hutoa tuzo katika kutambua michango unaotolewa na viongozi wa bara la Afrika katika kuleta maendeleo na utendaji wa kazi wenye ufanisi' katika kukuza uchumi kwa kusaidia kukuza na kuwainua wawekezaji wazawa. African Leadership ilishawahi kutoa tuzo kama hilo kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka April 9, 2014 katika hotel ya St Regis ya Washington, DC. Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production, New York.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akifuatilia hafla ya utoaji tuzo kwa viongozi wa Afrika iliyofanyika siku ya Alhamisi Sepemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis New York. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akielezea mafanikio na utendaji wa benki ya CRDB na jinsi gani inavyowawezesha wawekezaji wazawa kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu katika kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akitunukiwa tuzo na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
kushoto ni Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akisalimiana na Rais wa Malawi Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika mara tu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei kupokea tuzo iliyotolewa na African Leadership siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis, New York. kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akifuatilia sherehe ya Tuzo kutoka kwa African Leadership iliyofanyika katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.
Hapa ni siku Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye, alipomkabidhi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni