Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiongea na wasanii wa mkoa wa Arusha waliouthuria semina ya Ujasiriamali iliyofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi ya Arusha School iliopo jijini hapa
Wasanii wa aina mbalimbali wakiwa wanamsikiliza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa makini
Kaimu Afisa maendeleo ya Jamii Jiji Tajieli Mahega akiwa anasoma risala fupi inayoelezea lengo la kuandaa mafunzo hayo kwa wasanii hao
Kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Rebeka Mongi akiwa anaongea na wasanii wa mkoa wa Arusha waliouthuria mafunzo hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha
Wasanii wa mkoa wa Arusha pia waliatumia fursa hiyo kumkabidhi mkuu wa mkoa huu Mrisho Gambo baadhi ya kazi zao ambazo wamezifanya ili nayeye azione na aweze kuwasadia zaidi
kila mmoja alionyesha kipaji chake msanii huyu alionyesha kipaji cha kuimba
Mwenyekiti wa Shirikisho la waigizaji wa filamu jijini Arusha(TDFAA) Isack Chalo akiwa anaimba moja ya nyimbo zake alizozirekodi
wasanii walionyesha ujuzi wa aina mbalimbali kila mtu na kipaji chake
Na Woinde shizza,Arusha
SHIRIKISHO la wasanii wa filamu jijini Arusha washukiwa na Neema kutoka kwa Mkuu wa mkoa huo kutokana na mkuu huyo wa mkoa kuhaidi kutatua matatizo yao .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameahidi kuwasaidia wasanii wa filamu Mkoani hapa ambapo amewataka kufika ofisini kwake mapema kesho kwaajili ya kuwasikikiza na kutatua kero zao.
Akizungumza Jana katika ufunguzi wa Mafunzo yaliyoandaliwa na jiji hilo ya siku mbili yenye lengo la kuwafundisha vijana ujasiriamali na jinsi ya kujikwamua katika umaskini Gambo aliwataka vijana kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na asilimia tano inayo toka serikalini.
" Tunaamini serikali yetu imekusudia kuwasidia wanyonge na wote wenye juhudi katika utafutaji hivyo ni vyema mkachangamkia fursa zitolewazo katika jamii yenu na mjiunge katika vikundi ambapo mtanufaika. alisema Gambo.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la waigizaji wa filamu jijini Arusha(TDFAA) Isack Chalo alisema tasnia ya usanii mkoani hapo inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo ukosefu wa Eneo la kufanyia mazoezi na Television ya mkoa ya kuonyesha kazi zao.
" Tunatamani kupata eneo la kufanyia shughuli zetu hususani mazoezi kwani tulizoea kufanyia shule ya msingi makubusho ambapo kwa sasa tumefukuzwa , hatuna sehemu ya Uhuru kufanyia mazoezi yetu" alisema Chalo.
Alisema walikuwa wamepanga kujenga Meru Village sehemu ambapo wangepata uwanja mpana wa kufanyia mazoezi lakini hadi sasa hawajafanikiwa kutokana na kukosa sapoti.
"Kama vile wasanii wa Dar es salam walivyopatiwa eneo kule Bagamoyo na sisi tunapenda tukumbukwe katika hili ili tuwe huru katika kufanya shughuli zetu pamoja na pia tuweze kutambulika" alisema.
Aliwataka wana Arusha kununua kazi za wasanii wa Arusha na wasiegemee tu upande mmoja wa filamu za Kikorea ( seasons) wakawasahau watu wa nyumbani jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya wasanii Arusha na Tanzania kwa ujumla. Naye Mmoja wa wasanii hao Experinsia Musa akisoma risala mbele ya Mkuu wa mkoa alisema pamoja na kupatiwa eneo la kujenga ofisi zao, bado wanakabiliwa na eneo la kilimo na ufugaji kwa wale wasanii wasiokuwa na ajira ili waweze kujiajiri kupitia kilimo na ufugaji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni