Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ( kushoto ) akifurahia jambo leo wakati wa kufungua mafunzo ya Mgambo Kata ya Wasa na kata ya Kihanga.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela leo amefungua mafunzo ya Mgambo Kata ya Wasa na kata ya Kihanga karibu wana mgambo 170 wameanza rasmi mafunzo, pamoja na mambo mengine watajifunza uzalendo, mbinu za kivita,utawala na usalama wa raia.
Mh Kasesela amesisitiza suala la usafi, kuacha ulevi, kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii na kuwa mwamminifu.
Akimkaribisha Mkuu wa wilaya, Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Iringa Lt. Col. Kitta alisistiza kuwa wanaojifunza mgambo wana fursa nyingi sana za ajira hivyo basi wajitahidi wote wamalize mafunzo.
Mafunzo hayo mpaka sasa katika wilaya ya Iringa yapo Kata ya Wasa, Kihanga, Mboliboli na manispaa ya Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ( mwenye kaunda suti ) akipokea taarifa kabla ya kufungua mafunzo ya Mgambo Kata ya Wasa na kata ya Kihanga
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiongea wana mgambo 170 leo akifungua mafunzo ya Mgambo Kata ya Wasa na kata ya Kihanga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni