Aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki
amerejea nchini humo kimya kimya akitokea nchini Afrika Kusini
alipokuwepo kwa karibu wiki tatu akipatiwa matibabu.
Ripoti zimeeleza kuwa Kibaki
aliambatana na watu wa karibu wa familia yake na madaktari kutoka
Johannerburg aliwasili katika uwanja wa ndege wa Jumo Kenyatta
jumapili majira ya saa nne usiku.
Jana na leo rais huyo wa zamani
alitumia muda wake akiwa nyumbani kwake Muthaiga akiwa na wanafamilia
wa karibu pamoja na wadogo zake.
Kwa mujibu wa chanzo kutoka familia
ya Kibaki, kimesema familia yake ilitaka arejee kimya kimya bila ya
kuutangazia umma.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni