Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi,Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa bodi mpya.kesho.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira leo itazindua bodi mpya yake iliyoteuliwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge Julai Mosi mwaka huu baada ya ile ya awali kumaliza muda wake ambayo ilidumu kwa kipindi cha miaka mitatu.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ambayo inatarajiwa kuanza asubuhi.
Akizungumza jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa halfa hiyo pia itatumika kutambua na kupongeza juhudi zinazofanywa na bodi,menejimeni na wafanyakazi wa mamlaka hiyo. |
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni