Mabingwa watetezi Real Madrid
wametikisa nyavu mara mbili katika dakika mbili za mwisho wakitokea
nyuma na kuibuka na ushindi wa wa magoli 2-1 Sporting Lisbon katika
mchezo wao wa mwanzo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Sporting Lisbon iliongoza kupitia
shuti la chini la Bruno Cesar lakini Cristiano Ronaldo alisawazisha
katika dakika 89 kwa shuti kali la mpira wa adhabu, na kisha baadaye
Alvaro Morata akafunga la pili kwa kichwa.
Katika michezo mingine ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya timu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani ilitoa kipigo
kikali cha magoli 6-0 dhidi ya Legia War, huku Juventus ikitoka sare
ya 0-0 na Sevilla.
Bruno Cesar akishangilia goli baada ya kutikisa nyavu za Real Madrid
Cristiano Ronaldo akipiga mpira wa adhabu uliotinga wavuni na kuisawazishia Real Madrid goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni