Wananchi wa kata ya Mboliboli wamkisikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya Iringa wakati akiongea na wananchi hao
Wilaya ya Iringa inaanza kufanya sensa ya mifugo katika wilaya nzima. Zoezi hilo litaanza tarafa ya Pawaga na Idodi kuanzia tarehe 28 mwezi huu 9 na linategemea kuisha tarehe 15mwezi wa 10.
Akizindua sensa hiyo katika kata ya Mboliboli tarafa ya pawaga, Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alisema “ kila mwenye nmifugo ya aina yoyote lazima ahakikishe inahesabiwa kwa nia moja tu ya kupanga mipango endelevu ya kilimo na ufugaji katika wilaya yetu”.
Alisistiza pia sensa hii itasaidia kujua takwimu halisi. Wenyeji wa kata ya Mboliboli wamepokea zoezi hilo kwa mikono miwili na kusema hili ndio suluhisho la migogoro ya wakulima na wafanyakazi.
Tarafa za Pawaga na Idodi ndio zinaongoza kwa kuwa na mifugo mingi mkoa wa iringa , pia zina changamoto kubwa ya mashamba ya wakulima kuvamiwa na mifugo.
Zoezi hilo litaendeshwa na watendaji wa vijiji ambapo litasaidia kupanga utaratibu mpya wa ufugaji wenye tija. “ Huu ni wakati muafaka wa kuacha kuangalia idadi ya mifugo badalayake tuangalie thamani ya mifugo tulio nayo”
Wananchi pia walitoa kero zao ikiwemo maji ambayo yanasumbua, jengo la shule kuonyesha nyufa kutokana na upepo mkali, pia suala la mfereji wa umwagilaji ambao unahitaji kiasi cha shilingi bilioni 5 kurekebishwa.
Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti wa kijiji cha Migoli Mh Bosco Myombani alisema suala la mifugo ni jema sana kama tutakuwa na takwimu sahihi. Pia aliomba wadau wajitokeze kuchangia shule pamoja na miundombinu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni