SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi
utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale
katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandariya Tanga nchini
Tanzania.
Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao
cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo (tarehe 29 Septemba, 2016)
Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi
huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema
ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa
kukamilika mwaka 2020.
Amesema ujenzi wa bomba hilo
unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake
Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania.
Mradi huom kubwa utatekelezwa kwa
ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya
Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania
na Uganda.
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa bomba
hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa kusafirisha mapipa
200,000 kwa siku ambapo kila pipa litaliingizia taifa Dola za
Marekani 12.2.
Amebainisha kuwa pamoja na
kusafirisha mafuta ya kutoka nchini Uganda bomba hilo pia
linatarajiwa kusafirisha mafutakutoka nchi nyingine zaJ amhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na Sudani Kusini ambazo zimeonesha nia ya
kusafirisha mafuta yao kupitia bandari ya Tanga.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja
faida nyingine ambazo Tanzania itazipata kutoka na namradi huo kuwa
ni kupatika na kwa ajira zaidi ya 15,000 wakati wa ujenzi na ajira
2,000 baadaya ujenzi kukamilika, kuimarika kwa mahusiano ya
kidiplomasia, kukuza biashara katika ukanda wa kaskazini mwa
Tanzania, kampuni za ujenziza Tanzania kupata kazi za ujenzi.
Aidha, amesema Tanzania inatarajia
kunufaika zaidi kwa kutumia bomba hilo kupitisha mafuta
yanayotarajiwa kupatikana katika maeneo ya ziwa Tanganyika na Ziwa
Eyasi.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, SEPTEMBA 28, 2016
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni