Mkutano uliandaliwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wa wadau wa utalii walikutana kujadili changamoto na Tathimini zinazokabili sekta hiyo .
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya
Arusha Gabriel Fabian Daqarro wakifatilia mjadala uliokuwa ukiendelea
Katika mkutano huo pia wakuu wa wilaya zote zilizopo ndani ya mkoa wa Arusha waliuthuria. Na Woinde Shizza,Arusha
Wadau Wa utalii wameitaka serikali kuweza kuainisha kodi zote na kuweka katika mfumo mmoja ili kuweza kuepuka usumbufu unaojitokeza Mara kwamara pindi wageni wanapokuwa katika matembezi yao.
kodi hizo waotozwa katika sehemu mbali hususa ni katika mageti ambayo wanaingilia watalii mbugani kwani hivi sasa kumekuwepo na kodi nyingi ambazo zinaleta usumbufu kwa wageni ambapo wanasimamishwa kila mahali kwa mud a mrefu na kushindwa kufurahia utalii wanaoukuja kuufanya nchini hapa..
Hayo yameelezwa na mwenyekiti Wa chama cha wasafirishaji Wa utalii (TATO) wilbroad chambulo wakati akiongea katika kikao cha wadau wa utalii kilichoandaliwa na mkuu Wa mkoa Wa Arusha cha kujadili changamoto na Tathimini zinazokabili sekta hiyo .
Aliongeza kuwa mgeni anapofika nchini anatakiwa kupokelewa kama mfalme sio kusumbuliwa kwa kuwekwa mda mrefu katika viwanja vyetu vya ndege kwani inawakatisha tamaa na kujutia kuja kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini.
"Unakuta mgeni anakuja akifika kiwanja cha ndege anakaa zaidi ya lisaa limoja na nusu kwenye foleni akisubiria visa kweli huu ni usumbufu ,tunatakiwa mgeni akija hapa tumpokee kwa tabasamu ikiwezekana tumtandikie zulia jekundu ili akienda kwao atangaze nchi yetu na utalii wetu kwa ujumla "alisema Chambulo.
Pia aliitaka serekali ifatilie na ishughulike na utozwaji Wa ada za kodi zinazotozwa na mageti ya wilaya ya Monduli pamoja na geti la wilaya ya ngorongoro.
"Serekali na Wadau wote tunatakiwa kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama Wa watalii na Mali zao unaimarishwa zaidi"alisema
Kwa upande wake mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa mkutano huo ameuita ilikuwaleta pamoja kushiriki na kujadili namna gani watakuza utalii na kuboresha utalii katika mkoa Wa Arusha kwa ujumla na iwapo watashirikiana kwa pamoja itasaidia pia kukuza mapato na kuwa maradufu zaidi
.
Alisema nivizuri Wadau Wa utalii wakashirikishwa kwa mabadiliko yoyote ya ongezeko la kodi ili baadae kusiwepo na malalamiko ya kuegemea upande mmoja.
Aliongeza kuwa wao kama mkoa wanamkakati Wa kifunga CCTV katika maeneo mbalimbali ya mkoa ili kuzibiti uhalifu wanaofanyiwa watalii au wageni wanaotembelea mkoa wetu pamoja na vivutio vilivyopo Mkoani apo.
Katika mkutano huo mambo mambali mbali yaliathimiwa ikiwemo kuitaka serekali na Wadau Wa utalii kuweka mikakati ya ulinzi na usalama pamoja na kuangalia jinsi ya kuzuia ujangili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni