Leicester City imeifunga Porto
katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wakiwa nyumbani na
kuendeleza wimbi la ushindi katika ligi hiyo.
Alikuwa Islam Slimani, ambaye
anarekodi ya kuifunga Porto akiwa na klabu yake ya zamani Sporting
Lisbon, ndiye aliyefunga goli pekee kwa kichwa akiunganisha kona ya
Riyad Mahrez.
Kwa matokeo hayo Leicester
wanaongoza kundi F kwa tofauti ya pointi mbili ikifuatiwa na FC
Copenhagen, ambapo watakutana Oktoba 18.
Islam Slimani akipiga mpira wa kichwa ulioenda kujaa wavuni
Riyad Mahrez akipiga mpira wa adhabu kwa shuti la kuzungusha
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni