Mchezaji Charlie Austin amefunga
goli lake la tano katika michezo minne wakati Southampton ikiiadhibu
West Ham kwa magoli 3-0 ikiwa ni kipigo cha nne mfululizo cha Ligi
Kuu ya Uingereza.
Austin alikuwa wa kwanza kuifungia
Southampton kufuatia shambuli kali na kisha Dusan Tadic akaongeza la
pili akipokea pasi ya Austin na kumzungusha Adrian kabla ya kutikisa
nyavu.
James Ward-Prowse alikamilisha
karamu ya magoli kwa kufunga goli la tatu kwa shuti la chini na
kuiacha West Ham ikiwa haijapata ushindi wowote katika dimba lao
jipya la London.
Mshambuliaji Charlie Austin akiachia shuti lililojaa wavuni
Dusan Tadic akiwania mpira ambao alifanikiwa kumzidi maarifa kipa Adrian na kuandika goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni